Volgende

139. Kisimamo (Kusimama) (2) - Sheikh Abdul Majid

0 Bekeken· 17/07/15
Imam Hussain Foundation
0
In

Kisimamo kinachoambatana na rukuu ni wajib rukn kwa maana kwamba lau kitaachwa kisimamo hiki kwa makusudi au kusahau, swala itakuwa batil. Lau mukallaf atasahau kurukuu na akakumbuka kuwa kasahau rukuu kabla hajaweka paji lake la uso ardhini kwa ajili ya sijda, atanyanyuka, asimame wima kisha afanye rukuu na aendelee na swala. Kwa kuwa kisimamo kinachoambatana na Rukuu ni rukn, haitajuzu kwake kwenda rukuu moja kwa moja bila kusimama wima. Ni sharti katika kisimamo kwamba miguu yote miwili iwe imekita imara kwenye ardhi. Uchezesha viungo vya mwili kama vidole katika swala, kwa ajili ya ada au ungonjwa, haidhuru swala. Swala haibatiliki kwa vitendo hivi ijapokuwa ni bora kuepuka inapowwezekana.

Laat meer zien

 0 Comments sort   Sorteer op


Volgende